Home » » DK.KAMANI :WATANZANIA DUMISHENI SERIKALI MBILI

DK.KAMANI :WATANZANIA DUMISHENI SERIKALI MBILI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Dk.Titus Kamani.
 
Waziri  wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,  Dk.Titus Kamani, amewataka Watanzania kudumumisha Muungano wa serikali mbili kwa kile alichodai kuwa waasisi wa taifa la Tanzania, ahyati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume, walikaa na kuona mbali juu ya kuwa na Muungano wa aina hiyo.
Dk. Kamani aliyasema hayo juzi katika mapokezi ya pikipiki ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka mkoani Mara na kuingia mkoani Simiyu.

Lengo la mbio hizo ni kuwaunganisha vijana na wananchi kwa ujumla kuwa na ushirikiano na kuleta amani na utulivu  nchini.

Alisema busara za waasisi hao za kusisitiza Muungano zilizofanya kuundwa kwa muundo wa serikali mbili, zimesababisha hali ya amani, muungano wenye heshima na wa kuigwa barani Afrika kwani mpaka sasa ni Muungano imara na umefanikiwa kuleta amani kati ya Watanzania wote.

Dk. Kamani ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, alisema wapo watu ambao kupitia katika siasa, wanajaribu kuubeza Muungano ambao sasa unatimiza miaka 50 kwa sababu ya maslahi yao.

Dk. Kamani ambaye pia ni Mbunge wa Busega, alisema Bunge la Katiba kwa sasa limejikita katika kujadili mambo ya Muungano, lakini upande wa vyama vya upinzani kupitia Ukawa, vinataka kuwapo kwa serikali tatu bila ya kuthamini na kutokutambua hekima na busara za waasisi wa Muungano kwa Watanzania.

"Kwa sasa jicho la Watanzania linatazama Bunge, lakini utashangaa kuwaona na kuwasikia wabunge kutoka vyama vya upinzani wanapoingia bungeni kuanza kupinga serikali mbili licha ya kuwa wapo ndani ya kamati zao wao hukubaliana na serikali mbili na kuwapo kwa Muungano," alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa