Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WADAU wa afya katika Halmshauri ya Mji wa Bariadi, mkoani Simiyu,
wameridhia kutumika kwa mfumo mpya wa utoaji wa huduma za afya kwa kadi
(TIKA).
Wadau hao walifikia uamuzi huo jana kwenye warsha iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Bariadi.
Mbali na kuridhia kutumika kwa mfumo huo ambao uko chini ya Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wadau hao wamedai ili kupatikana
mafanikio ya kutumika kwa mfumo huo ni vema kuwepo kwa usimamizi
mkubwa wa fedha zitakazotokana na huduma hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, walisema uanzishwaji wa Tika
utasaidia wananchi kutibiwa kwa uarahisi kuliko ilivyo sasa ambapo
huangaika katika kutafuta fedha za matibabu.
“Tunaipongeza serikali kwa kuleta mfuno huu, kwani unalenga kutatua
kero waliyonayo ya kila siku katika kupata huduma za afya,” alisema
Selina Deusi.
Akitoa maelezo ya juu ya faida ya mfumo huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF, Elltruder Mbogolo, alisema lengo la kuletwa kwa mfumo
huu ni kupunguza kero za upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba
katika vituo vya afya na hospitali.
Akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Katibu
Tawala wa mkoa huo, Mwanvua Jirumbi, amewataka viongozi wa halmashauri
zote kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mradi huo, ili uweze kuwanufaisha
wananchi.
Chanzo;anzania Daima
0 comments:
Post a Comment