Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Akizungumza kwa niaba ya ukoo huo na Tanzania Daima, jijini Dar es
Salaam juzi, John Ileme, alisema Mei mwaka jana, Mabiti alijitawaza kuwa
Mtemi wa Dutwa kupitia mgongo wa jamii ya Wasukuma wachache wa ukoo wa
Bahunda kinyume cha utamaduni wa jamii hiyo.
Alisema wanamtaka afanye hivyo kwa sababu ukoo wa Dutwa haumtambui
kuwa ni mwanaukoo, na kwa utaratibu wa mila na desturi hana sifa ya kuwa
mtemi wa utemi huo.
Ileme alisema endapo atashindwa kufanya hivyo kwa hiari yake, Chifu
wa Dutwa na ukoo wa Bahunda wa Dutwa hautasita kuchukua hatua za
kisheria, ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani.
Chaanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment