Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alisema kwa kiwango kikubwa Haki za Binadamu zilizoainishwa kwenye Rasimu ya Katiba zinafanana sana na namna zilivyo kwenye katiba ya sasa isipokuwa zimeongezwa nyingine chache.
Alisema kuwa kwa kuzingatia maoni ya wananchi ya kutaka kuimarishwa kwa kwa haki za binadamu, Tume imependekeza kuimarishwa kwa haki hizo kwa kuondoa vikwazo visivyokuwa vya lazima.
“Kwa mfano, ili kuimarisha ushiriki wa wananchi kwenye uongozi tumependekeza kuruhusu mgombea huru kikatiba,” alisema Jaji Warioba.
Alisema kuwa kwa kuzingatia maoni ya wananchi na mikataba ya kimataifa Tume imependekeza kuongezwa kwa haki nyingine mpya kwa kuzingatia maadili ya kitanzania.
Haki hizo mpya kuwa ni Haki za Wafanyakazi, Haki ya Mtoto, Haki ya Watu wenye Ulemavu, Haki za Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Vijana, Haki za kupata Habari na Haki na Uhuru wa Vyombo vya Habari.
“Ingawa baadhi ya haki hizo zimo kwenye sheria mahususi za nchi, Tume imeona ni vyema zikawekwa kwenye katiba ili kuweka msingi wa wananchi kuweza kuzihoji na kudai utekelezaji wake kikatiba,” alisema Jaji Warioba.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment