Home » » TIMUA TIMUA YA WALIMU MASWA YAIKERA CWT.‏

TIMUA TIMUA YA WALIMU MASWA YAIKERA CWT.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399

Na Samwel Mwanga-Simiyu.
CHAMA Cha Walimu(CWT)Mkoa wa Simiyu kimeonyeshwa kukerwa na tabia ya
Idara ya Utumishi ya Walimu(TSD) kuwafukuza walimu mara kwa mara
katika wilaya ya Maswa mkoani humo badala ya kutoa adhabu mbadala.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CWT mkoani humu,Kulwa Dwese jana
katika mkutano mkuu wa kawaida wa chama hicho wilayani Maswa
uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Maswa.
Chama hicho kimeshauri TSD kutoa adhabu mbadala kama vile kuzuia
mishahara,kutowapandisha madaraja ni adhabu tosha kwa walimu
wanaoajiriwa badala ya kukimbilia kuwafukuza kazi na utumishi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wengi wa walimu wa shule za msingi na
sekondari wanaotimuliwa kazi ni vijana ambao alidai hawazijui vyema
sheria za kazi, si wavumilivu kwa kutopita hata JKT, na kuwa wamekuwa
wakifanya kazi katika mazingira magumu ikilinganishwa na matarajio yao
ya ,Matokeo Makubwa sasa, "Big Reasult Now".
Kufuatia hali hiyo CWT mkoani hapa kimesema,kinatafakari kuonana na
waziri wa Utumishi wa umma kuangalia upya adhabu za kuwafukuza walimu
katika wilaya hiyo ambayo ni moja ya wilaya zinazokabiliwa na upungufu
wa walimu na hata kufanya vibaya katika ufaulu wa mitihani.
Awali Katibu Idara ya Utumishi ya Walimu(Nidhamu)wilayani humo ,Hezron
Rhodes, aliwaambia wajumbe wa mkutano huo ambao ni wawakilishi wa
walimu sehemu ya kazi kuwa katika kipindi cha mika mitatu hadi sasa
walimu 50 wa shule za msingi na sekondari wamefukuzwa kazi na idara
hiyo huku wengine 15 wakisubiriwa kupewa barua za kutimuliwa kazi
wilayani humo.
Alisema sababu kubwa za kutolewa adhabu hizo ni utoro kazini na
kuendelea kupokea mishahara halali bila kufundisha,ulevi wa kupindukia
saa za kazi,wajibikaji na nidhamu mbaya ikiwemo lugha za chafu na kuwa
walivumiliwa kwa muda mrefu kwa kupewa maonyo ya mara kwa mara bila
mafanikio na hata kufikia hatua hiyo.
Alisema wengi waligundulika kuwa wameajiriwa sehemu zingine kamna
kutoa mfano wa baadhi yao kuajiriwa katika taasisi mbalimbali na hivyo
wakiendelea kupokea mishahara miwili.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Efrem
Lema alionya kuwepo kwa matukio ya walimu na wanafunzi kugombea
wapenzi kwa maana ya walimu wa kiume au wa kike na wanafunzi wa kike
au wa kiume mashuleni.
"kuna mchezo mchafu unaofanyika hapa wilayani Maswa utakuta wanafunzi
wanagombania wapenzi shuleni ambao ni walimu wa kiume na walimu wa
kiume kugombania wapenzi wanafunzi wa kike hii si tabia nzuri lazima
tuikomeshe na hatutasita kuwachukulia hatua walimu wenye tabia hiyo
chafu"alisema.
 Kuhusu madai yao kwa mwajiri aliwataka walimu kuwavumilivu wakati
serikali ikikusnaya nguvu za kuwalipa madai na mapunjo ya stahili zao
mbalimbali.
Awali Afisa Elimu Msingi wilaya ya Maswa Saimon Mabeyo alisema kuwa
halamshauri hiyo imeanza kuwaipa walimu na kila fedha ya matumizi
mengine ya Idara na kuwalipa walimu na hadi sasa wameshalipa kiasi cha
shilingi 9,977,240/= kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Februari
mwaka huu.
Naye Katibu wa mkoa wa CWT Fatuma Bakari amewaonya walimu juu ya tabia
ya kulipua ufundishaji mashuleni kwa kutumia mtindo auliopewa jina la
"ufundishaji wa Luku" kwa maana ya mwalimu kufundisha pale tu
anapokuwa amepata mshahara na asipokuwa na mshahara hafundishi
ipasavyo.
Katibu huyo pia amewaagiza walimu viongozi wawakilishi sehemu za kazi
kuwaelimisha walimu wenzao juu ya sheria,nidhamu na kubaini kasoro
zilizopo na kutoa ushirikiano sehemu ya kazi kwa mwajiri na CWT kwani
wapo walimu wengine hujikuta wakifukuzwa kazi kwa kutojua sheria.
Alisema maovu yote na utovu wa nidhamu kwa walimu daima hugunduliwa na
walimu hao amabo ni viogozi sehemu za kazi hivyo ni wajibu wao kuona
hali ya nidhamu na uwajibikaji inakuwepo mahali pa kazi ikiwemo kudai
ni wagonjwa na kuuguliwa kwa waganga wa jadi bila kwenda hospitali na
bila ya hati ya matibabu(Sick Sheet).

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa