Halmashauri ya mji wa Bariadi katika mkoa wa Simiyu imefanikiwa kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano ambao unatarajiwa kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa lengo la kuboresha huduma na maisha ya wakazi wa mji wa Bariadi.
Akizindua mpango huo mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. Paschal Mabiti amesema matumizi ya mfumo wa mpango mkakati ulianza rasmi kutumika hapa nchini mwaka 2002 ambapo mfumo huo umeonyesha kuzaa matokeo mazuri pale unapotekelezwa vizuri.
Mheshimiwa Mabiti ameongeza kuwa mfumo wa mpango mkakati unalenga kupima utendaji katika wizara,Idara zinazojitegemea na mashirika ya umma na kwamba mfumo huu unatoa kipaumbele katika matumizi ya rasilimali ambazo kwa kawaida ni chache kuliko matumizi.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Bariadi Bw. Robert Lweyo amesema lengo mahususi la mpango mkakati wa Halmashauri ya mji wa Bariadi nikuboresha huduma na kuinua uchumi wa wa wananchi wa mji wa Bariadi ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya mji wa Bariadi kwa ujumla.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima akifunga mjadala wa majadiliano ya mpango huo amewataka wadau wote walioshiriki katika kutengeneza mpango mkakati huo kushirikiana pia katika utekelezaji wake kwani umegusa maeneo mengi yanayohusisha sekta mbali mbali.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment