
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
Wakati mtumishi huyo Lawrence Kileo ambaye ni Afisa Wanyamapori Mwandamizi wa Pori hilo akisimamishwa kazi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Nyalandu alisema jana kuwa pia ameiagiza mamlaka husika kukamilisha uchunguzi haraka na kumchukulia hatua za kinidhamu Afisa Wanyamapori wa Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, Benjamin Mkasamali, anayetuhumiwa kuwatorosha majangili ambao waliwinda wanyamapori wasioruhusiwa kuwindwa.
Kusimamishwa kazi kwa afisa huyo kumekuja siku tano baada ya kusimamishwa kwa watumishi wengine 21 wa Idara ya Wanyamapori wa maeneo tofauti kusimamishwa kazi.
Januari 8, mwaka huu, Wizara ya Maliasili na Utalii iliwashimamisha kazi watumishi hao ambao haikuwataja kwa majina, kwa kuwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa ujangili, rushwa na hujuma.
Alisema Mkasamali anachunguzwa baada ya wizara kutumia njia za kiintelijinsia imebaini aliingilia kati na kuwaachia huru majangili waliokamatwa na Kikosi cha Doria cha Kampuni ya Friedkin Conservation Fund, waliokuwa wamewinda tohe 12 (madume matano na majike saba) ambao hawakuwepo katika orodha ya leseni yao ya uwindaji.
Pia majangili hao waliua wanyamapori wengine wanne aina ya insha wanaojulikana kwa jina la kitaalamu kama oribi.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment