Meatu. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu, mkoani Simiyu, wameomba Bodi ya Pamba kuweka utaratibu wa
kusambaza mbegu mbadala ya zao la pamba, baada ya zilizosambazwa na
Kampuni ya Quton kubainika hazioti katika maeneo ya wilayani hapa.
Wakichangia hoja kuhusu maandalizi ya kilimo msimu
wa mwaka huu kwenye kikao cha Baraza la Madiwani juzi, madiwani hao
walisema mbegu za Quton zilizopigiwa debe kuwa ni ubora zimegoma kuota
katika maeneo mengi.
Kutokana na hali hiyo, walisema kuna kila sababu
ya bodi ya pamba hivi sasa itafute mbegu mbadala ili kuwezesha wakulima
kuwahi kupanda kabla ya Desemba 20.
Walisema bila kuchukuliwa hatua, vinginevyo hali ya kilimo cha pamba msimu huu itakuwa mbaya.
Walisema mbegu hizo zilizopandwa baada ya kuitikia
wito wa viongozi zimekataa kuota katika kata za Mwabusalu, Mwanyahina,
Mwabuzo, Imalaseko na Nkoma.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment