Na Derick Milton, Simiyu
SHIRIKA la World Vision Tanzania limekabidhi mradi
mkubwa wa maendeleo kwa wananchi wa Kata za Nkoma na Mwalushu wilayani Itilima
mkoani Simiyu uliodumu kwa miaka 16 ambao umenufaisha wananchi 49,608.
Mr a d i h u o amb a o umekabidhiwa mwishoni mwa
wiki kwa wananchi ukiwa chini ya Halmashauri ya wilaya hiyo ulianzishwa mwaka 1998
ukiwa na lengo la kuongeza ustawi kwa watu maskini hasa ustawi wa watoto ukiwa
chini ya shirika hilo kwa ufadhili wa watu wa nchini Newzeland.
Akitoa ufafanuzi juu mafanikio ya mradi huo tangu
kuanzishwa kwake hadi kumalizika Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania,
Dkt. Kasilima Yosh alisema kuwa mradi huo ulikuwa na lengo kuu moja kuleta
ustawi kwa kila mtoto.
Al i s ema mr a d i wa m a e n d e l e o N k o m a
ulianzishwa mwaka 1998 ambapo hadi kufikia mwisho wake umeweza kuleta maendeleo
kwa wananchi katika nyanja za kiuchumi, kiafya, kijamii, kiulinzi, pamoja na
kimaamuzi na haki zao kwa ujumla.
Alisema katika idadi hiyo ya wananchi walionufaika
na mradi huo wanawake ni 13,273, huku wanaume wakiwa 14,335, watoto wakiwa
jumla yao 22,956, wa v u l a n a 1 0 , 9 5 5 n a wasichana wakiwa 12,001.
Alisema katika mafanikio ya mradi huo kwa upande wa
sekta ya kilimo na uhakika wa chakula shirika hilo limefanikiwa kuunda vikundi
120 vya wakulima wanaotumia njia nbora za kilimo, matumizi ya mbolea, pamoja na
uzalishaji wa mazao umeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Aliongeza wakulima wanaotumia njia bora za kilimo
wameongezeka kutoka asilimia 7 mwaka 1998 hadi kufikia asilimia 47 kwa mwaka
huu, ambapo katika sekta ya afya jumla ya wahudumu wa afya 32 wamepewa mafunzo
ya kuhudumia jamii katika huduma za afya.
Alibainisha magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na
maji nayo yamepungua kutoka asilimia 87 hadi kufikia asilimia 24 kwa mwaka huu,
ikiwa pamoja na kupungua kwa utapiamlo mkali na wa kati kwa watoto chini ya
miaka 5 kutoka 42 miaka 0.6 na ule wa kati kutoka asilimia 25 hadi kufikia 0.
Aidha alisema katika upande wa elimu katika mradi
huo shirika limefanikiwa kujenga jumla ya madarasa 55, kwa kushirikiana na
Serikali kukarabati madarasa 9, nyumba 2 za walimu, ofisi 16 za walimu nazo
zimejengwa na mradi, vitabu 3,850 vimetolewa kwa shule 11, pamoja na kutoa
madawati 1,126 kwa shule 11.
Akipokea
mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti ambaye pia alikuwa mgeni rasmi
alilipongeza shirika hilo kwa kazi hiyo kubwa ikiwa pamoja na kuwataka viongozi
wa halmashauri kuhakikisha mradi unakuwa endelevu pamoja na kutunzwa.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment