Mwandishi wetu, Maswa-Simiyu Yetu
Mamlaka ya Mji mdogo katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa
imeamua kuwaondoa Wafanyabishara kwa nguvu katika maeneo ambayo hayaruhusiwi
kufanya Biashara kwa mujibu wa Sheria ndogo ndogo za Mji huo
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya
Mji mdogo Maswa Bibi Veronica Nestory wakati akiongea na Radio Free Africa
Mjini Nyalikungu Maswa leo
Bibi Veronica pamoja na mambo mengine amesema Mamlaka yake
imeunda timu ya Watalaamu wa Mamlaka wanao simamia zoezi la kuwaondoa Wafanya
biashara kwa msaada wa walinzi wa amani (Polisi) kwa ajili ya Wafanyabishara
Ambao wamendelea
kukaidi amri halali iliotolewa na Mamlaka kwa muda mrefu ya kuwataka kuondoka
maeneo yasiyo ruhusiwa kuendesha biashara kinyume cha sheria na kwenda kufanyia
shughuli zao katika maeneo waliopangiwa na Mamalaka yake
Kaimu Afisa Mtendaji huyo ameyataja maeneo hayo kuwa ni
pamoja na kuzunguka eneo la uwanja michezo nguzo nane, Njiapanda na eneo la
Binza kwa ajili ya kuoshea magari
Aidha akibainisha zaidi kuwa Wafanya bishara watakoa husika
na oparesheni hiyo kuwa ni Mafundi Baiskeli,Wauza mitumba,wauzaji wa vifaa vya
ujenzi kama vile mbao,Saruji,Nondo,mabati vitu vingine ni Chokaa weld meshi na
Wenye magereji ya Magari na Pikipiki
Amesema zoezi hilo ni endelevu na amewaonya watu wakao puuza
agizo hilo Mamalaka ya yake haitasisita kuwafikisha katika vyombo vya Dola ili
mkondo wa sheria upite
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment