na Edna Bondo
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, amesema Tanzania imekubali kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Kukuza Kilimo katika nchi za Afrika (AGRA), litakalofanyika kati ya Septemba 26 hadi 28 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Chiza alisema kongamano hilo litafanyika mji mdogo wa Ngurdoto, mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi wa kimataifa, litajadili sera ya mapinduzi ya kijani.
Alisema jukwaa hilo pia litajadili na kutafuta njia bora za kuboresha kilimo barani Afrika na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kwa kushirikiana na vyama vya ushirika pamoja na wadau wengine.
Chiza alibainisha kuwa mjadala huo utatoa njia bora za matumizi ya rasilimali na kukabiliana na changamoto zinazowakabili mamilioni ya wakulima katika Bara la Afrika.
“Lengo kuu la serikali ni kuijenga Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, kwa kiasi kikubwa na kukua kwa sekta ya kilimo,” aliongeza Chiza.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment