Home » » DUNIA INAELEKEA WAPI? AMFUMA MKEWE AKIZINI NA MTOTO WAO, AWAUA

DUNIA INAELEKEA WAPI? AMFUMA MKEWE AKIZINI NA MTOTO WAO, AWAUA


Na Mwandishi Wetu, Simiyu
AMA kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Msemo huu unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mkazi mmoja wa Kijiji cha Nghoboko wilayani Meatu mkoani hapa, Stephano Mihilu mwenye miaka 60, kudaiwa kumfumania mkewe wa ndoa akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa.


Taarifa za kipolisi zilizotua kwenye dawati la Amani zinadai kuwa tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa Julai 22, mwaka huu ambapo baada Stephano kulishuhudia tukio hilo, aliwaua mama na mwanaye kwa kuwacharanga mapanga bila huruma.



“Jamaa aliporudi nyumbani, aliingia ndani na kukutana na tukio ambalo hakuwahi kulifikiria, alimkuta mkewe akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa, nadhani akili ilihama, akachukua panga na kuwacharanga wote mpaka walipokata roho,” alisema afande mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwani si msemaji wa jeshi la polisi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa