Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Raisi
utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi
Elizabeth Arthy akizungumza mbele ya makamu wa Rais juu ya mchango wa
serikali ya Uingereza katika kuboresha elimu.
Mkuu
wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi
Elizabeth Arthy akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya
msingi Gamondo A iliyoo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Bibi Elizabeth Arthy alipotembelea shule ya msingi Gamondo A mkoani Simyu, kuona utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania.
Uwekezaji
katika sekta ya elimu Nchini kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu
(EQUIP-Tanzania) ambao umelenga kuboresha mchakato wa kufundisha na
matokeo ya kujifunza kwa watoto nchini umeweza kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa Mkoani Simiyu.
Uwekezaji
huo ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia Wizara ya
Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) umeleta ufanisi wa elimu na
kufanya viwango cha ufaulu kuwa juu kutoka asilimia 36 mwaka 2013 mpaka
asilimia 68 2017.
Na
katika kutimiza hayo Jumla ya kiasi cha shilingi Bil 1.7 kutoka DFID
kupitia mradi wa kuinua ubora wa Elimu Nchini (Equip) zimetolewa kwa
Serikali ya Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu
ya elimu Mkoani humo .
Akizungumzia
nia ya serikali ya Uingereza wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan , Mkuu
wa DFID-Tanzania Elizabeth Arthy alisema wametoa kiasi hicho cha fedha
kwa serikali ya Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya
miundombinu iliyopo.
Arthy
alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho kinatarajiwa kutumika katika
kuboresha miundombinu hiyo na kujenga vyumba vya madarasa, ofisi za
walimu pamoja matundu ya vyoo kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta
ufanisi wa utoaji elimu kwa walimu na wanafunzi.
Mkuu
huyo alieleza kuwa tangu shirika lake lianze kusaidia katika Elimu
,Mkoa wa Simiyu umeweza kupata mafanikio makubwa na ya haraka ambayo
yamesaidia kuuweka Mkoa katika nafasi nzuri Kitaifa katika matokeo ya
mitihani ya kuhitimu elimu ya Msingi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka aliuelezea mpango wa kuinua ubora wa
elimu Tanzania kwa Mkoa wake kuwa ni mpango ambao umeweza kuleta
mabadiliko makubwa ya kukuza viwango vya ufaulu wa wanafunzi.
Mtaka
anaeleza wanalishukuru shirika la maendeleo ya uingereza (DFID) kupitia
mpango wa kuinua ubora wa elimu kwa kuona kuwa Tanzania na Mkoa wake
unahitaji msaada huo wa kuinua kiwango cha ufaulu pamoja na uboreshaji
wa mazingira ya elimu.
Amesema
kupitia msaada huo wa fedha kiasi cha shilingi Bil 1.7 zilizotolewa
kwao na shirika la DFID kwa mwaka huu za kuboresha mazingira ya elimu
,zitawasaidia kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambavyo
vyote hivyo ni changamoto kubwa Mkoani kwake.
Anaongeza
kuwa kupitia fedha hizo anaanimi tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa
na matundu ya vyoo utapungua kwa kiasi kikubwa na kwamba atasimamia
vema fedha hizo ili ziweze kutumika ipasavyo.
0 comments:
Post a Comment