Na: Lilian lundo - MAELEZO
Serikali
ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza ikiwa nchi inakabiliwa na janga la
njaa na wala si taasisi, asasi za kiraia au wanasiasa.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo wakati wa mahojiano
na mwandishi wa habari hii alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mijadala
mbalimbali inayoendelea katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba
Tanzania imekabiliwa na tatizo la njaa.
Cheyo alisema kuwa, huwezi kusema nchi ina njaa wakati vyakula vipo katika masoko mbalimbali hapa nchini.
Amewataka watanzania kutofautisha kupanda kwa bei za vyakula na janga la njaa.
Aidha,
Cheyo alisema kuwa tatizo hilo tayari limetatuliwa na Serikali kwa
kutoa tani milioni 1.5 za mahindi ambazo zitasambazwa nchi nzima kwa
ajili ya wananchi kununua.
Aliendelea
kwa kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mahindi hayo kuuzwa kwa
uangalifu kwani gharama yake itakuwa ni ya chini, hivyo kuna watu ambao
watajitokeza kununua kiasi kikubwa na kwenda kukihifadhi kwa ajili ya
kukiuza kwa gharama ya juu baadae.
Vile
vile aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kutunza vyakula badala ya
kuuza vyakula vyote mara wanapovuna, ili vyakula hivyo viweze kuwasaidia
pale ambapo mvua zinakuwa zimechelewa kama ambavyo imekuwa kwa mwaka
huu.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment