Na Jovina Bujulu
MAELEZO
Dar es Salaam
IMEELEZWA
kuwa kuanzishwa kwa mfuko wa mafunzo wa habari uliopo katika muswada
wa sheria ya huduma za habari utasaidia kuibua weledi, stadi, ujuzi, na
ubobeaji kwa waandishi wa habari katika utelekezaji majukumu yao ya kila
siku.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustino, Dkt. Samwilu Mwaffisi wakati alipokuwa akizungumzia
kuhusu maudhui yaliyopo katika muswada wa huduma za habari.
“Naunga
mkono uanzishwaji wa mfuko wa mafunzo ya wanahabari kwa asilimia 100
isipokuwa mafunzo hayo yajikite katika mafunzo ya vitendo zaidi kuliko
nadharia, kwani vyuo vingi tulivyonavyo nchini vinafundisha zaidi
nadharia” alisema Dkt. Mwaffisi.
Akifafanua
zaidi alisema kanuni zitapotungwa katika uendeshaji wa mfuko huo mkazo
wake uelekezwe katika mafunzo zaidi, ambapo wanahabari wanaosomea
shahada mafunzoyao yaanze mwaka wa kwanza wa masomo yao na baada ya
kuhitimu shahada ianzishwe sheria ya kusoma kwa vitendo kwa kipindi
fulani.
Aidha
Dkt. Mwaffisi alisema kuwa ni vyema mfuko wa mafunzo ukawajengea uwezo
wanahabari katika ubobezi wa fani tofauti tofauti na hivyo kuwapa uzoefu
wa kuandika fani kwa weledi zaidi.
Akizungumzia
kuhusu Bodi ya ithibati inayothibitisha wanahabari, Dkt. Mwaffisi
alisema jambo hilo limekuja wakati mwafaka kwani itamfanya mwandishi
awajibike kwa jamii.
“Uthibitishwaji
wa wanahabari utawafanya waandike kwa weledi na ufanisi zaidi
wakizingatia maadili ya taaluma na jamii ili kuepuka adhabu ambayo
wanaweza kupewa na bodi ya ithibati iwapo watavunja maadili” aliongeza
Dkt. Mwaffisi.
0 comments:
Post a Comment