Home » » MEATU WANUFAIKA NA MFUKO WA JIMBO

MEATU WANUFAIKA NA MFUKO WA JIMBO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Samwel Mwanga-Meatu
 
WANANCHI wa jimbo la Meatu katika mkoa wa Simiyu wamenufaika na mfuko
wa jimbo hilo kufuatia vikundi  20 na miradi 13 mbalimbali kuwezeshwa
kiasi cha fedha shilingi 47,175,000/=kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.
 
Hayo yalielezwa jana na Mbunge wa Jimbo la Meatu,Meshack
Opolukwa(CHADEMA) wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mfuko huo
kwa kipindi hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja
vya Stendi mjini Mwanhuzi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
 
 Alisema kwa kipindi hicho mfuko huo ulipokea kiasi cha fedha shilingi
54,142,310/= kutoka serikalini katika kipindi hicho ambapo mwaka wake
wa fedha unaishia Juni 30 mwaka huu.
 
“ndugu wananchi nataka niwaeleze kuwa  mfuko wa jimbo la Meatu katika
kipindi hiki cha fedha 2013/2014 kitakachomalizika Juni 30 mwaka huu
tulipokea kiasi cha fedha shilingi 54,142,310/= katika mfuko wa jimbo
la Meatu na fedha hizi zinatolewa na serikali ili kuchochea maendeleo
ya wananchi katika jimbo”alisema.
 
Alisema kuwa kwa kupitia kamati ya mfuko huo akiwa Mwenyekiti waliweza
kupitia maombi mbalimbali ya vikundi na miradi  ya wananchi wa
jimbo hilo waliomba kuwezeshwa lakini waliweza kuviwezesha vikundi
hivyo bila ubaguzi wa aina yoyote ya kiitikadi
 
“mfuko huu ni wenu wananchi na hizi fedha ni zenu mie mbunge ni
msimamizi tu na  unawawezesha wote ili mradi mkiwa katika vikundi vya
kufanya  shughuli ambazo ni halali za kuwaletea maendeleo wala
haubagui itikadi ya kisiasa ya mtu kama wewe ni CCM,UDP,CHADEMA au CUF
na umekidhi vigezo vilivyowekwa unawezeshwa”alisema huku akishangiliwa
na umati wa watu.
 
Pia alitaja baadhi ya vikundi na miradi iliyowezeshwa na kiasi cha
fedha katika mabano kuwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya kilimo cha
umwagiliaji maji kwa vikundi 10 ambavyo kila kimoja kimepata pampu
moja ya kusukuma maji yenye thamani ya shilingi 475,000/=
 
Alivitaja vikundi hivyo ni pamoja na Iramba
ndogo,Mwagwila,Mwamanonu,Itaba,Mkombozi
Itaba,Ikingijo,Mwamishali,Ushirikiano Mwamishali,Bukundi na Mwanhuzi.
 
 
Vikundi 10 vilivyopatiwa mbuzi 20  kila kimoja  kwa thamani ya
shilingi 25,000 kila mbuzi ni pamoja na
Mshikamano,Mkombozi,Mwamanongu,Utulivu(Mwamanongo,)Mwanjolo,PangaSawa,Idoselo,Mwamalole,Mwangudo,
na Kimali.
 
Miradi  mbalimbali 13 iliyotumia kiasi cha fedha Shilingi
13,825,000/=katika sekta ya elimu na ujenzi ambapo ilihusika na
utengenezaji wa madawati katika shule za msingi na afya  hususani
ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Usiulize.
 
Miradi mingine na thamani yake katika mabano ni katika shule ya msingi
Anex(Tsh 850,000/=),Shule zilizopatiwa madawati 20 kila mmoja kwa
thamani ya shilingi 2,400,000/= ni pamoja na
Mwafuguji,Kadondo,Chambala, Mwagwila na Ngungulu.
 
Shule nyingine  zilizopatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za
walimu ni pamoja na  Shule ya awali Mwaghalanja(Tsh
2,000,000.=),Mwanjolo(Tsh 2,500,000/=),Mwamishali(Ts
1,800,000/=),Ujenzi wa kivuko  cha darajaMwanyahina(Tsh
8,000,000/=),Ujenzi wa ofisi ya Mtendaji wa kijiji Mshikamano(Tsh
1,800,000/= na Utengenezaji wa majiko sanifu katika shule za msingi
10(Tsh 3,800,000/=)
 
Aidha Mbunge huyo alilalamikia kitendo cha baadhi ya viongozi wa
serikali na kisiasa wilayani humo ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu
kuhakikisha wanakwamisha shughuli zake hasa za kutimiza ahadi zake
alizozihaidi kwa wananchi akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo,Rosemary
Kirigini ambaye pia ni mbunge wa viti maalum.
                                                 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa