Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
siku chache baada ya naibu waziri tawala za mikoa na serikali za mitaa tamisemi agrey mwanri kutoa siku 30 kwa mkandarasi kwilasa investment kukamilisha barabara hadi sasa hakuna kinachoendelea.
naibu huyo alitoa agizo hilo alipoafanya ziara wilayani bariadi mkoani simiyu kuwa ndani ya siku 30 barabara hiyo iwe imekamilika na kuanza kupitika.
agizo hilo lilitolewa na waziri mwanri baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wanaopakana na barabara kuwa kasi ya ujenzi wake imekuwa hairidhishi.
barabara hiyo ni ya kiwango cha lami yenye urefu wa mita 700,licha ya kuanza siku nyingi kujengwa hadi sasa bado haijakamilika.
kutokana na hali hiyo mkuu wa wilaya hiyo erasto sima ameuagiza uongozi wa halmashauri ya mji kumchukulia hatua mkandarasi huo.
0 comments:
Post a Comment