Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
madiwani
wa halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani simiyu wamelalamikia kitendo cha
askari wa usalama barabarani kuwakamata watu wanaosafirisha abiria
kwa pikipiki (bodaboda) kinyume cha sheria.
hayo
wameeyaeleza leo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika
ukumbi wa barideko mjini bariadi.
wamelalamikia
kitendo cha askari wa usalama barabarani kuwakamata bodaboda kinyume na
taratibu za jeshi la polisi.
wameeleza
kuwa baadhi ya askari hao wamekuwa wakikaa katika maeneo yasiyo rasmi na kisha
kuwasimamisha waendesha bodaboda hali ambayo imekuwa
ikisababisha ajali na majeraha kwa wahusika.
akijibu
malalamiko hayo mkuu wa wilaya hiyo erasto sima ambaye ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalam ya wilaya amelaani kitendo hicho na kuahidi kulifuatilia
ikiwemo kutoa mafunzo kwa waendesha bodaboda wote.
amewataka
pia askari wa usalama barabarani kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za kazi
yao
0 comments:
Post a Comment