Na Samwel Mwanga, Simiyu.
MKUU wa mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amewaijia juu viongozi wenye
tabia ya kujisifu na kujigamba kuomba chakula cha msaada toka
serikalini pale wanaposhindwa kutekeleza agizo la serikali la kulima
mtama na wananchi wao kujikuta wakikabiliwa na njaa.
Mabiti ambaye alionyesha kukerwa na tabia ya kuwa omba omba wa chakula
serikalini alisema, baadhi ya viongozi,watendaji na wananchi mkoani
hapa wamepuuza agizo lake la kuhimiza wananchi kulima zao la mtama
ambalo linalostahimili ukame,.
Kufuatia kuwepo kwa hali hiyo Mkuu huyo wa mkoa ameagiza kila mkuu wa
wilaya na mkurugezni wake Mtendaji wa halmashauri za wilaya na
mji,kuanzia wiki hii kuana kugawa mbegu za mtama aina ya "WAHI" inayo
komaa haraka kufuatia hali halisi ilivyo hivi sasa.
Mkuu huyo aliyasema hayo mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati ya
ushauri ya mkoa katika ukumbi wa mikutano wa BARIDECO mjini Bariadi,
na kuwaagiza wakuu na wakurugenzi wote wa wilayani wanapokwenda
vijijini kuhimiza kupanda mtama kuongozana na gari lenye mbegu za
mtama wa aina hiyo ili kuwagawia wananchikuepuka visingizio kuwa
hawana mbegu.
Akitoa agizo hilo Mkuu huyo alidai kuwa hali ya hewa si rafiki mkoani
Simiyu,kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,ambapo baadhi ya maaeneo
hayana mtawanyiko mzuri na mvua za vuli zinazonyesha lakini baadhi ya
maeneo wananchi wake kwa mara nyingine wanakabiliwa na njaa baada ya
kutozingatia maagizo na ushauri wa kupanda mazao yanayostahimili ukame
hasa mtama na ya jamii ya mizizi hasa viazi vitamu.
Akifungua kikao hicho kinacho jumuisha wakuu wa wilaya,
wabunge,wenyeviti na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya
na mji,sekreterieti ya ushauri ya mkoa,wadau wa maendeleo Mkuu huyo
alisema, licha ya mkoa kuwa na azimio la pamoja kwa kila kaya kulima
ekari mbili za mtama lakini baadhi ya viongozi,watendaji na wananchi
wamepuuza agizo hilo na sasa mkoa unakabiliwa na njaa.
Huku akilaani na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi wa siasa wenye
tabia ya kujigamba kuomba chakula cha msaada na kujivunia wananchi wao
wanapopelekewa chakula cha msaada kwa vile wanakabiliwa na njaa na
chakula kinapowafikia wao hujisifu kwa kazi nzuri na eti ni kiongozi
bora.
"moja ya kazi mbaya ni siyo ipenda ni kuomba omba chakula cha njaa
kutoka serikalini,inashangaza kuona baadhi ya viongozi
hujitapa,kujisifu kuomba chakula cha msaada na kuingiza siasa katika
suala la njaa kamwe sipendi viongozi wa aina hiyo kujivunia
kuwapelekewa wananchi wao chakula cha msaada eti wana njaa' alisema.
"hali ya hewa 2014 si rafiki katika mkoa wa Simiyu,kutokana na
mababadiliko ya tabia nchi,pamoja na kupitisha azimio la wananchi
kulima mtama bado wananchi wameendelea na kupendela kupanda mahindi
katika maeno ambayo hayafai kwa kustawisha zao hilo na sasa kuna
njaa'alisema mkuu huyo.
Mkuu huyo alisema mkoa wa Simiyu unaweza kuondokana na aibu ya kuwa
ombaomba ya chakula kwa kuiga moja ya mkoa jirani wa Singida ambayo
miaka ya 80 na 90 ulikuwa ukikabiliwa na njaa ya mara kwa mara na
sasa mkoa huo unauza hata akiba yake kwa wananchi wa mikoa jirani
ukiwemo mkoa wa Simiyu.
Kufuatia hali hiyo mkuu huyo ameziagiza halmashauri zote kuhakikisha
zoezi hilo la kulima mtama kwa kila kaya lina fanikiwa na kuwa kaya
isiyo lima ekari mbili za mtama na viazi vitamu na baadaye kuripotiwa
kuwa ina njaa kamwe isiorodheshwe kuuwa ina njaa na haitapewa chakula
cha msaada kwa watu watakao kabiliwa na njaa.
Alisema sasa mkoa wa Simiyu utaandaa na kuandika kiatabu maalum cha
mwongozo wa kilimo kwa viongozi wa ngazi zote mkoani hapa
kitakachoelezea kilimo cha mazao ya chakula na biashara na kuiagiza
sekreterieti ya ushauri ya mkoa huo ndani ya miezi miwili kiwe tayari.
Kwa mujibu wa taarifa za ofisi ya mkoa tathimini iliyofanyika mkoani
hapa mwezi oktoba 2013 imebainika kuwa wananchi wapatao 511,386 katika
vijiji 345 katika kata 76 wana upungufu wa chakula na wanahitaj jumla
ya tani 28,900 za chakula na tani 7,225 za chakula aina ya mikunde
ambazo zinahitajika hadi ifikapo mwezi machi mwaka huu.
Mkuu huyo pia amewaagiza wataalam wa kilimo na maafisa ugani wote
mkoani hapa kufanya tahathimini ndani ya wiki mbili kubaini maeneo na
athari juu ya mbegu ya pamba aina ya Quton isiyo manyoya ni kwa nini
haikuota na imeathiri kwa kiwango gani malengo ya mkoa huo unaozalisha
asilimia 42 ya pamba yote nchini.
Mkuu huyo pia ameziagiza halmashauri za wilaya na mji katika mkoa huo
kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepuka migogoro ya
wafugaji na tabia ya wafugaji ya kuhama hama.
Home »
» MABITI AWACHARUKIA VIONGOZI NA WATENDAJI
MABITI AWACHARUKIA VIONGOZI NA WATENDAJI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment