Home »
» MWANRI AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA H/SHAURI
MWANRI AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA H/SHAURI
NAIBU
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw.Aggrey Mwanri ,
amemsimamisha kazi Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima,
mkoani Simiyu, Paschal Manyama.
Bw. Mwanri alichukua uamuzi huo
baada ya kubaini kuwa, mradi wa barabara inayoingia katika Ofisi za
halmshauri hiyo yenye kilomita 1.03, imejengwa chini ya kiwango.
Barabara
hiyo imejengwa na Mkandarasi Virgin Company Limited ambayo ujenzi wake
uligharimu zaidi ya sh. milioni tisa bila kuweka mitaro na baada ya
kuulizwa na Bw. Mwanri, hakuwa na jibu la kuridhisha.
Wakati
akiendelea kukagua mradi huo, alibaini kuwepo kasoro nyingi ikiwemo ya
mkandarasi huyo kutopewa mkataba na mchoro unaonyesha gharama za mradi
(BOQ).
Bw. Mwanri alipata mashaka na utendaji kazi wa mhandisi huyo
kutokana na majibu yake kutokuwa ya kitaalamu na kumwagiza Katibu Tawala
Mkoa, Mwanvua Jilumbi kumwondoa katika nafasi aliyonayo na kumtafutia
kazi nyingine.
"Namsimamisha kazi huyo mhandisi, hafai hata kidogo
kuwa katika nafasi hii ndiyo maana nauliza maswali yanamshinda, kama
ataendelea kukaa hapa, halmashauri itapata hasara.
"Katibu Tawala Mkoa tafuta mtu mwingine na huyu mhandisi mpangieni kazi nyingine si hii,"
alisema
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment