
TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi inahudumua barabara zenye urefu wa jumla ya km 607.49. Hayo yamesemwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne, kilichofanyika tarehe 30/7/2024 ndani ya ukumbi wa halmashauri, kijiji cha Isenge.Akiwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Meneja TARURA, Mhandisi, Khalid Mang'ola amesema kwa km 607.49, barabara za Mkusanyo ni km 199.79, barabara za Mlisho ni km 353.23 na barabara za Jamii ni km 54.47. " Kati ya barabara hizo km 224.77 sawa na 37% zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka, km 219.54 sawa na 36.14% ni za wastani na km 163.18 ambazo ni 26.86% ziko katika hali mbaya na zinapitika kwa shida...