Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa(hawapo pichani) Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani wa Kata ya Dutwa Wilayani Bariadi, Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Igaganulwa Kata ya Dutwa (hawapo pichani) Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kijijini hapo wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amepiga marufuku Halmashauri zote
Mkoani humo kutoza ushuru wa biashara ndogondogo zinazofanywa na
wananchi kwa kutandika na kupanga bidhaa zao chini au kuuzwa katika
mabeseni maarufu kama matandiko.
Mtaka
ametoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Igaganulwa,
Mhe.Nhandi Masaka Kachala na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko yao
kuhusu ushuru huo, wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la
kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .
Amesema
suala hilo lilishatolewa maelekezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, hivyo Halmashauri zinapaswa
kubuni vyanzo vipya vya mapato vyenye tija kwa Halmashauri na wananchi
badala ya kutegemea kutoza ushuru unaowakwaza wananchi.
“Kama
kuna Halmashauri bado inatoza ushuru wa matandiko wamechelewa sana,
kuanzia kesho hamna huo ushuru, kama ninyi mnafikiri mapato ni kutoza
tandiko la nyanya, dagaa, mchicha na ninyi kama wakuu wa idara hiki
ndicho chanzo mnachokifikiria kichwani hiyo kazi haiwafai, mkatafute
kazi nyingine ya kufanya” alisema Mtaka.
“Halmashauri
lazima ibuni chanzo cha mapato chenye tija kwenye Halmashauri na watu.
Sasa mtu anahangaika na beseni lake la nyanya wewe unamtoza ushuru,
umechangia nini, beseni si lako nyanya si zako” alisema Mtaka.
0 comments:
Post a Comment