Mkoa
wa Simiyu ni miongoni mwa mikao 12 ya Tanzania inayoendelea na zeozi la
kuwasajili wananchi kwa lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.
Kwa
sasa zoezi hilo limeingia kwenye awamu ya pili ya Usajili katika wilaya
zote za mkoa huo ambazo ni Bariadi, Meatu, Busega, Maswa na Itilima
huku mwitikio wa watu ukiwa mkubwa.
wanaoshiriki kwenye zoezi hilo ni wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wageni na Wakimbizi.
Pichani ni Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwachukua alama za Kibaiolojia wananchi wa mkoa wa Simiyu Kijiji cha Mwakiboro wakati zoezi la Usajili likiendelea .
Zoezi la Usajili likiendelea katika Kijiji cha Kilulu wilayani Bariadi
Wananchi wa Kijiji cha Mwakiboro mkoani Simiyu wakisubiri kupatiwa huduma ya Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa.
0 comments:
Post a Comment