Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi,
watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum
cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa,
Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani
Meatu.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na viongozi,
watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum
cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa,
Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani
humo
Baadhi
ya viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji
na wadau mbalimbali wa uhifadhi wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa
zikijadiliwa katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo
katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Meneja
wa Pori la Akiba la Maswa, Lusato Masinde akiwasilisha taarifa yake kwa
viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na
wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la
kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Katibu
wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori ya Makao, Robert Simon
akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na
Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao
maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la
Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao
wilayani Meatu.
Mhifadhi
kutoka Ranchi ya MWIBA, Julius Makaroti akiwasilisha taarifa ya ranchi
hiyo kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya
Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha
kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi
ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
……………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameitaka Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Meatu mkoani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya
hiyo,Dkt. Joseph Chilongani kutekeleza kwa weledi, uadilifu na haki
zoezi la kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi litakaloanza September
04, 2017.
Mtaka
ametoa kauli hiyo mara baada ya viongozi wa Serikali na Chama Mkoa na
Wilaya, Wataalam, wafugaji na wadau wa uhifadhi na Utalii kukutana na
kujadili suala la uondoaji mifugo katika Maeneo ya Hifadhi, yakiwemo ya
Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori (WMA) Makao wilayani Meatu.
“Mkafanye
zoezi hili kwa weledi mkubwa na haki, lisije likawa zoezi la kuwaonea
watu, kufanya utapeli kwa kujifanya mnachukua ng’ombe kwa ajili ya
kutaifisha halafu mkagawana; viongozi na wote mtakaohusika mkalisimamie
kwa makini sana suala hili” alisisitiza Mtaka
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu Mhe.Joseph Chilongani amesema baada ya makubaliano
yaliyofikiwa kati ya viongozi, wafugaji na wadau wa uhifadhi na utalii
ametoa muda wa siku nne na kufikia Septemba 04 mwaka huu, wafugaji wawe
wametoa mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa hiari.
Dkt.Chilongani
amebainisha kuwa Viongozi wa Wilaya ya Meatu walikutana na wafugaji
katika maeneo yao na kuwatahadhalisha juu ya uingizwaji wa mifugo kwenye
maeneo ya hifadhi, ili kuwasaidia waepuke adhabu ya kifungo na mifugo
yao kutaifishwa kwa kuwa kuingiza mifugo hifadhini ni makosa kwa mujibu
wa sheria.
“Maandalizi
yote yako tayari, timu za kutekeleza zoezi hili zote zipo, nitoe muda
wa siku hizi zilizobaki ili kufikia Jumatatu ya tarehe 04 zoezi la
kuondoa mifugo kwenye Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na WMA ya
Makao lianze, tulishawapa wafugaji muda wa kutosha tulipokuwa tukipita
kwenye vijiji kuzungumza nao juu ya madhara ya kuingiza mifugo
hifadhini” amesema.
Kwa
upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Maswa Lasato Masinde amezitaja
baadhi ya changamoto za kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi kuwa ni
ushindani wa malisho na maji kati ya wanyamapori na wafugwao,ongezeko
la ujangili, kuuwawa kwa wanyamapori hasa walao nyama, magonjwa na
mmonyoko wa udongo kutokana na wafugaji kukata miti.
Aidha,
Masinde amefafanua kuwa suala la uingizwaji wa mifugo katika hifadhi
linachangiwa pia na baadhi ya viongozi wa vijiji wasiokuwa waadilifu
ambao hupokea fedha kwa wafugaji na kuwaruhusu kuingiza mifugo yao,
jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amemuagiza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Meatu kuwachukulia hatua stahiki wale
wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito
kwa wafugaji kupima maeneo yao wanayomiliki na kuyawekea miundombinu ya
mifugo kama vile visima vya maji na mabwawa, majosho na mashamba ya
malisho ili waweze kufuga kisasa na kuondokana na adha ya kuhangaika
kutafuta maji na malisho.
Katika
kikao hicho wafugaji kwa pamoja wamekubali kutoa mifugo katika maeneo
ya hifadhi na kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa
kupima maeneo yao na kuweka miundombinu, hivyo wameomba watalaam wa
Ardhi na Mifugo waweze kuwasaidia namna wanavyoweza kutumia maeneo yao
kufuga kisasa.
0 comments:
Post a Comment