Home » » HATARI. MWANAMKE AUAWA, AZIKWA CHOONI

HATARI. MWANAMKE AUAWA, AZIKWA CHOONI

 na Samwel Mwanga,
 Maswa NGOLO Soni (45) mkazi wa kijiji cha Jihu, kata ya Badi, wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, ameuawa kwa kunyongwa na kisha mwili wake kuzikwa katika shimo la choo kijijini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na diwani wa kata hiyo, Martine Masele (CHADEMA), na kuthibitishwa na polisi wilayani Maswa, tukio la kuuawa kwa mwanamke huyo lilitokea Novemba 4 mwaka huu. Taarifa hizo zinaeleza zaidi kuwa kabla ya kugundulika kwa mauaji hayo, marehemu alikuwa akiishi peke yake na kutoweka nyumbani kwake tangu Oktoba 2, mwaka huu, hadi mwili wake ulipopatikana siku ya tukio. Awali ilidaiwa kuwa marehemu alikuwa akifanya biashara ya kununua mifugo na kuiweka kwa kaka zake ambao wanadaiwa kufanya unyama huo. Katika taarifa hiyo Masele alisema mara baada ya kumuua kwa kushirikiana walimzika marehemu katika shimo la choo nyumbani kwa rafiki yao aliyetajwa kwa jina moja la Zabron kijijini humo kwa miadi ya kumpatia sh milioni sita. Alisema walishindwa kutimiza ahadi yao na hivyo siri ya mauaji hayo kuvuja na taarifa kutolewa jeshi la polisi wilayani hapa ambalo liliufukua mwili wa marehemu. Kutokana na mauaji hayo, Jeshi la Polisi Maswa linawashilikia watu wanne wakiwemo kaka wa marehemu ambao ni Wilson Soni (45), Majilia Soni (42) na Mbilo Soni (32) pamoja na rafiki yao Zabron na wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika wa mauaji hayo. 
Chanzo: Tanzania Daima  

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa