Na Samwel Mwanga-Meatu
MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Meatu mkoa wa
Simiyu,John Wanga amekanusha madai kuwa amemsimamisha kazi Mwalimu
Koraba Baruti wa shule ya msingi Mwanyahina aliyewawakilisha walimu
kutoa kero mbalimbali za walimu wilayani humo wakati wa ziara ya Naibu
Waziri wa Tamisemi,Aggrey Mwanri aliyoifanya katika wilaya hiyo hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Mwanhuzi
alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa habari hizo ambazo
zimeandikwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya malalamiko ya
mwalimu huyo.
Alisema kuwa walipokuwa katika kikao cha ndani cha majumuisho ya ziara
ya Mwanri aliyoifanya wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo ilitolewa fursa ya kuuliza maswali au kutoa kero
mbalimbali.
"ni kweli Mwalimu Baruti aliuliza maswali na kutoa kero mbalimbali
huku akidai anawawakilisha walimu na hiyo ni haki yake ya msingi tena
ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni yake na aliitumia vizuri lakini
Naibu Waziri alimtaka ampatie vielelezo ili kuthibitisha alichokuwa
ana kisema"alisema.
Aliongeza kueleza kuwa hajamsimamisha wala hafikirii kufanya jambo
lolote la kumsimamisha kazi mwalimu huyo kutokana na kutoa kero za
walimu kwa Naibu Waziri Mwanri.
'hapana mie siko hivyo sijamsimamisha mwalimu kazi kama inavyodaiwa na
wala sifikirii kufanya hivyo na pia sijatoa maelekezo ya kufanana na
hivyo eti kwa sababu ametoa kero mbele ya Naibu Waziri Mwanri hizo
habari ni za uzushi tu kama ipo barua ya namna hiyo basi aitoe
hadharani"alisema.
Katika Mitandao ya kijamii iliandika habari kuwa Mkurugenzi,Wanga
amemsimamisha kazi kwa barua Mwalimu Baruti aliyewakilisha walimu
kutoa kero mbalimbali za walimu wilayani humo kwenye kikao cha ndani
na Aggrey Mwanri mpaka atakaposibitisha tuhuma zote alizotoa.
Tuhuma ambazo alizitaja mbele ya Mwanri ni pamoja na walimu kutolipwa
fedha zao za likizo na Uhamisho na Mafaili yao kuandikwa Paid,huku
wakiambiwa pesa hakuna nasisitiza tuhuma hizi ni ukweli mtupu majina
ya walimu hao tunayo.
Walimu kucheleweshewa fedha za likizo hadi likizo imeisha na fedha
kutumika kwa mambo mengine pia kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya
ulipwaji wa stahili mbalimbali za walimu kutoka kwa Mkurugenzi huyo
aliyehamia wilani humo hivi karibuni.
Pia walimu walionywa kabla kutochangia wala kuongea lolote kwenye
kikao hicho la sivyo chamoto watakiona na limekuwa ni rungu kuzuia
Walimu kutohudhuria kikao chao na Mbunge wao Meshaki Opulukwa(Chadema)
alichopanga kifanyike januari 23 mwaka huu ili kusikiliza kero zao.
Home »
» MKURUGENZI MEATU AKANUSHA KUMSIMAMISHA MWALIMU ALIMUULIZA SWALI NAIBU WAZIRI MWANRI.
MKURUGENZI MEATU AKANUSHA KUMSIMAMISHA MWALIMU ALIMUULIZA SWALI NAIBU WAZIRI MWANRI.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment